Ni wazi kwamba kuna taarifa zingine za kimtandao ni siri, lakini licha ya hili ni wazi kwamba ni vizuri kwa mtu kufuta taarifa zake mara kwa mara pindi anapomaliza kutumia kompyuta
Taarifa hizi zinaweza zikawa kama ni nywila n.k. vile vile fikiria kwa mfano kama watu wanatumia kompyuta ya aina moja? hapa ndio jambo hili linazidi kuwa la muhimu zaidi kufuta taarifa hizo kila baada ya kutumia kivinjari.
Kama unatumia microsoft edge katika kompyuta yako basi leo TeknoKona inakujuza ujanja huu. Lakini kingine cha kujua ni suala la taarifa ambazo zitaweza futika: nazo ni
- kumbukumbu ya mitandao uliyopitia (mfano. www.teknolojia.co.tz) kupitia kivinjari
- kumbukumbu ya vitu ulivyoshusha (download) kupitia kivinjari
- Taarifa za ‘cookies’ na zingine zingie
- mafaili au picha ambazo zimejificha katiaka sehemu ambayo ni ngumu kuzipata kwa haraka (cached files & photos)
- neno siri (password) ambazo ulijaza katika mitandao mbali mbali wakati unatumia kivinjari
- taarifa ambazo huwa zinajijaza mara kwa mara (autofill form data)
- ruhusa za kimtandao (site permission)
Hapo awali ilikua kama unataka kufuta yote haya basi ulikua huna budi kwenda kufuta katika eneo la settings pindi tuu ukimaliza kutumia kivinjari. lakini vipi kama utaweza kufanya hivi wakati unamaliza tuu kutumia kivinjari chako cha edge?
Kwa kuanzia kabisa fungua kivinjari chako cha microsoft edge kwa kutumia kompyuta na kisha ingia katika vidoti vitatu kule upande wa juu
Ikishatoka window nyingine hapo ingia katika eneo la settings
Baada ya hapo ingia katika eneo la “Privacy, Search, and Services” kisha ingia katika eneo la “Clear Browsing Data” na ingia katika chaguo la “Choose What To Clear Every Time You Close The Browser” kisha fanya machaguzi
yatatokea machaguo mengi ambayo unaweza kuchagua, kila chaguo ambalo utachagua basi hii inamaanisha kuwa kila ukimaliza kutumia kivinjari cha edge kila unapokifunga basi kitakuwa kinafuta taarifa zote hizo ambazo umezijachua zifutwe.
Niambia hii umeipokea vipi? je njia hii ulikuwa unaijua? niandike hapo chini sehemu ya maoni, ningependa kusika kutoka kwako.
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Kivinjari Cha Edge Hapa
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
No Comment! Be the first one.