Vuta picha uko mbali kidogo na simu yako, na unaisikia kabisa inaita. Hapo kuna mawili unaweza ukimbilia na kuipokea lakini vipi kama mtu anaekupigia hana umuhimu sana?
Saa zingine unaweza ukaamua kuacha kupokea simu flani flani hivi kwa sababu uko bize tuu sasa vipi kama simu hiyo ikiwa ni ya maana zaidi?
Hapo ndipo uzuri wa Teknolojia unaopoonekana. Pata picha kama utakua mbali na simu yako na wakati inaita inataja kabisa na jina la mpigaji. Hii imekaa poa sio
KWA iOS
kitu cha kwanza kabisa ni kwenda katika ‘Settings’ kisha shuka mpaka katika ‘Phone’
Baada ya hapo ingia katika ‘Announce Calls’ chini ya calls na kisha chagua ‘Always’
KWA ANDROID
Kitu cha kwanza kabisa kufanya ni kuingia katika soko la Google PlayStore na kupakua App Ya Caller Name Talker
Ukishaipakua, ifungue App hiyo na kisha nenda katika eneo la “Lower ringtone volume” ambapo utaweza kupunguza sauti kidogo. kuwezesha kufanya hivyo kutakusaidia kusikia jina la mtu vizuri zaidi.
Baada ya hapo chezesha sauti na itakua vizuri ukiweka sauti ya “Talker Volume” ikiwa asilimia 100.
Ingia katika eneo la ‘Call Alert Settings” na kisha “Initial Time Delay” ili kuweka sekunde za jina hilo kutajwa pia unaweza ingia katika “Repeat Count” na “Alert Repeat Time Interval” ili kuweka jina hilo kurudiwa kulingana na mahitaji yako.
Watu ambao wanatumia Android toleo la Mashmello na kuendelea inawabidi waende katika eneo la Settings-> Accessibility na kisha wawashe chaguo la “Caller Name Talker” ili kuweza kutumia hii.
Mpaka hapo utakuwa mtaalamu wa swala hili. Kila jina ulisikia ukiwa unapigiwa simu. Itakuwa ni vizuri zaidi kuwahifadhi watu kwa majina ambayo kidogo yataendana na matamshi ya kizungu. Bila kufanya hivyo unaweza ukacheka sana!