Alama ya kuonesha upendo/kupenda/kukubaliana na tweet ya mtu yaani ‘favorite’ katika mtandao wa Twitter kubadilishwa.
Mtandao huo wa Twitter umetangaza rasmi leo hii ya kwamba watabadilisha alama hiyo na kuleta alama ya kopa – nyekundu.
Alama ya ‘favorite’ ya sasa katika mtandao wa Twitter ilikuja rasmi mwaka 2006 na ililenga kukuwezesha kuwekea katika tweet yeyote ambayo ungependa kuiona siku za mbele, na sasa wanataka maana kubwa kuwa ‘umependa’ tweet husika. Yaani kama vile ‘Like’ kwenye mtandao wa Facebook.
One Comment