Kulinda taarifa zako katika kompyuta yako sio kitu kidogo. Kinshitaji kuwa na programu au softwares mbalimbali za mbadala ili kuwezesha hili. Mara nyingi hatupendi taarifa zetu ziwe wazi hadharani ndio maana karibia vifaa vyetu vyote vya kielektroniki (simu janja, kompyuta n.k) tunavilinda na neno siri
Je unajua Jinsi ya kutengeneza nenosiri imara? kama ni mtihani soma hapa
Sawa unaweza ukajitahidi labda ukaficha baadhi ya taarifa zako kwa watu ambao sio wa karibu. Lakini vipi kuhusu watu wako wa karibu? Nazungumzia wale watu ambao wanajua neno siri la kompyuta yako. Vipi kama kuna baadhi ya ma’faili/folder hutaki wayaone? inabidi utumia njia mbadala sio/ kumbuka tayari mtu/watu hao wanalijua neno siri la kompyuta yako kwa ujumla
Kama hutaki waone folder husika (labda kuna suri zako au kuna vitu muhimu katika folder hilo) itabidi kutumia njia mbadala ili kuhakikisha vitu hivyo havitaonwa na mtu mwingine yeyote.
Watu wa karibu wanaweza pia wakawa ni wafanyakazi wenzio pale ofisini, au hata mtu anaefagiaga hapo ndani wakati ukitoka. Kumbuka watu hawa wanaweza wakatumia kompyuta yako ukiwa umetoka bila ya wewe kujua. hivyo wanaweza wakachukia taarifa ya muhimu yeyote bila kujua kwako.
Kuna njia maalumu ya kuhakikisha kuwa faili lako au hata folder halifunguliwi na mtu mwingine yeyote isipokuwa wewe tuu. Hii ni kwa kutumia ‘software’ inayoitwa Wise Folder Hider ambayo inatengenezwa au inatoka katika kampuni linaloitwa WiseCleaner
Ukishakuwa na Wise Folder Hider (WiseCleaner) unakuwa na uwezo wa kuficha faili au folder lolote. Cha kufanya ni ku “right click’ juu ya folder au faili hilo ili uweze lificha nyuma ya neno siri.
Kwa faili au folder unalohisi halipo kimaadili vizuri mtu hataweza kuliona tena na pia hata kama unahifadhi taarifa zako muhimu kama vile zile za kibenki ni vizuri kuweka ulinzi imara
MUHIMU: Kamwe usijiruhumu kusahau neno siri lako kwani hutaweza kuzipata tena taarifa zako za muhimu ulizozificha hapo mwanzo. Ni vizuri kulichagua neno siri ambalo utalikumbuka bila matatizo.
Software hiyo wanasema inapatikana katika Windows 8.1 au zile za nyuma lakini TeknoKona Imefanya majaribio na inafanya kazi kama kawaida katika Windows 10
Kwa wale watumiaji wa Windows kwa kutumia Pc zao itawabidi waingie hapa ili kushusha softaware hiyo na kuiweka katika PC zao tayari kwa kutumia.
WINDOWS – Wise Folder Hider
One Comment