Instagram imetangaza kuwa inafikiria nje ya box la mraba, sasa unaweza ukapakia picha zako katika mtandao wa instagram hata kama haziko katika mfumo wa mraba (square).
Walitoa maelezo zaidi katika ukurasa wao katika blog. Hata hivyo hii haitakua kwa picha tuu, hata video zako unaweza kuzipakia bila kujali kuziweka katika mfumo wa mraba —Fikiria nje ya box— hahaha!
Hii ni nzuri sio? maana kuna wengine picha mpaka watumia App za kuziweka katika mraba (kama vile InstaSize). Wengine wanalazimika kukata (Crop) kipande katika picha ambacho huenda kingebakia kingekuwa ni kumbukumbu tosha.

Fikiria mnapiga picha ya kundi alafu wakati  unaipakia katika mtandao wa instagram inakulazimu ukate baadhi ya watu ili picha ikubali kupakia, haivutii sio? hayo yote yamebadilika kutokana na toleo jipya la instagram Yaani instagram toleo (version) 7.5
Instagram toleo la 7.5 kwa ajili ya iOs linapatikana katika AppStore na instagram toleo la 7.5 kwa ajili ya Android linapatikana katika Google Play pia. Kama bado unatumia matoleo ya zamani basi haina budi wewe kuyapakua matoleo hayo mapya na ufurahie instagram kwa sura mpya
No Comment! Be the first one.