Teknolojia ya Fingerprint yashindwa kufanya kazi kwa usahihi kwenye baadhi ya simu maarufu za Samsung. Apps za huduma za kibenki zaanza kuzuiwa kufanya kazi.
Mabenki katika mataifa kama Uingereza, Marekani na China yaondoa apps zake kwenye simu za Samsung Galaxy S10 na Note 10 baada ya tatizo la kiusalama linalohusisha uwezo wa kufungua simu kw alama za vidole (fingerprint).

Kwa takribani wiki sasa imefahamika teknolojia ya kisasa inayotumika kwa ajili ya kutambua alama za vidole kwa simu za Galaxy S10 na Note 10 inaweza kujikuta ikikubali vidole ambavyo si sahihi au vya watu wengine kimakosa.
Good morning Robert, We’ve removed the app from the Play Store for customers with Samsung S10 devices. This is due to reports that there are security concerns regarding these devices. We hope to have our app available again shortly once the issue has been resolved. SY
— NatWest (@NatWest_Help) October 20, 2019
Apps za mabenki zimekuwa zikitengenezwa zikitegemea mfumo wa teknolojia ya utambuaji alama za vidole, mabenki yamechukua uamuzi huu kuepusha watu kuibiwa pesa iwapo watu wasiohusika wakiweza kuzifungua simu za wateja wao kutokana na tatizo hili.
Hilo limefahamika baada ya watumiaji kadhaa ambao walitumia viulinzi kioo – screenprotectors kwenye simu zao na wakajikuta mfumo huo wa ufunguaji kwa alama za vidole ambao upo kwenye kioo/display kujikuta haufanya kazi vizuri.
Teknolojia ya utambuaji alama za vidole kwa mfumo wa kugusa kioo (display) ndio teknolojia inayopendwa kwa sasa ili kuachana na teknolojia ile ya kuweka eneo spesheli hasa hasa nyuma ya simu.
Samsung wameshakubali uwepo wa tatizo hilo, wamehaidi kuleta sasisho jipya la programu endeshaji katika simu hizo ili kuondoa tatizo hilo. Tatizo hilo limekuwepo kwa watu wanaotumia screenprotector tuu.