Firefox ambayo ni kivinjari namba mbili kwa kutumiwa na watu wengi zaidi imekosekana katika soko la app la Apple kwa muda mrefu sana baada ya kutofautiana kisera na watengenezaji wa mfumo endeshi huo, hata hivyo Firefox wamejishusha na kukubali masharti ya Apple kwa watengenezaji wa apps.
Tofauti kubwa kati ya Firefox na Apple imekuwa katika ulazima wa kutumia teknolojia muhimu kwa ufanyaji kazi wa vivinjari (browser) za WebKit framework na ingini ya JavaScript ambapo Apple imelazimisha vivinjari vyote kutumia teknolojia za Apple katika utengenezaji wa vivinjari vya kutumika katika bidhaa zake – iPhone na iPad.
Apple inawanyima watengenezaji wote wa vivinjari (browser) uwezo wa kuvifanya vivinjari vyao viwe ndio chaguo namba moja, Apple wanafanya hivi ili kukilinda kivinjari chao ambacho ndio wanataka kiwe chaguo la kwanza kwa watumiaji wake. Mwanzoni Firefox walikataa kabisa kukubaliana na sharti hili na walisema kwamba Apple wanatakiwa kurekebisha sera zao ili ziweze kuruhusu vivinjari vya nje kuwa ndio chaguo namba moja.
Firefox imekuwa inapatikana kwa watumiaji wa Android kwa kipindi kirefu sasa, na sera za Apple kwa kipindi kirefu zimekuwa zikiwazuia Firefox kuingiza kivinjari hicho katika soko la Apple. Firefox inaingia katika soko la vitumizi vya Apple na kupambana na ushindani mkubwa unaotoka kwa vivinjari vya Safari na Chrome ambavyo vimekuwa sokoni kwa muda mrefu.
Endelea kutembelea mtandao wako namba moja Tanzania kwa habari na maujanja ya teknolojia.
One Comment