Kampuni maarufu katika utengenezaji wa diski uhifadhi ya SanDisk waja na Flash Diski ndogo kabisa yenye uwezo mkubwa wa uhifadhi kuliko kawaida. Diski uhifadhi hiyo inayokuja na jina la ‘The Ultra Fit’ inakuja na uwezo wa GB 128, ukilinganisha uwezo huu na umbo la diski uhifadhi hiyo ndio utagundua ni kwa kiasi gani teknolojia inazidi kufanya diski uhifadhi zizidi kuwa ndogo.

Kampuni ya SanDisk imetambulisha flash diski hiyo huko nchini Taipei na inategemea kuanza kuzisambaza katoko masoko yote duniani. Flash diski hiyo pia inakuja katika matoleo mengine matatu ya uhifadhi, kuna zenye GB 16, 32 na 64.
Imetengenezwa kwa teknolojia ya USB 3 na hivyo inakasi kubwa ya uhamishaji wa mafaili ukilinganisha na flash diski nyingi zilizopo kwenye soko ambazo bado zinatumia teknolojia ya USB 2. Wenyewe wanadai itaweza kuhamisha mafaili kwa kasi ya hadi MB 130 kwa sekunde.
Flash diski ya GB 128 inategemewa kuuzwa kwa takribani Tsh laki mbili (Dola 119.99 za kimarekani).
Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maunjanja ya kiteknolojia!
No Comment! Be the first one.