Mfumo-endeshaji wa Android una soko kubwa sana la apps linaloweza kukushangaza. Kila siku utakutana na kitu kipya ambacho huenda kikasuluhisha tatizo lako la siku nyingi.
Mfano ni app ya Flynx ambayo ni kivinjari kinachoelea kwenye skrini ya simu. App ya Flynx na app za aina yake zinakupa uhuru wa kufanya mambo mengine wakati unasubiria kurasa ya wavuti unayotaka kufunguka.
Pakua app hii kwenye Google Playstore kisha ifungue na kuingia kwa kutumia akaunti ya Google au barua-pepe. Kuingia kwenye app hiyo kutakusaidia pia kuhifadhi linki za mitandao unayotembelea na hivyo kuweza kuzifikia unapotaka.
Fungua linki yoyote ya wavuti kwenye app yoyote na utaulizwa kutumia Flynx mara moja au kuiweka kama chaguo la moja-kwa-moja. Chagua la moja-kwa-moja kufanya maisha yako yawe rahisi. Linki yako itafunguka kwenye ki-puto kinachoelea wakati unaendelea na mambo mengine. Kurasa ikimaliza kupakuliwa utaona kiputo kile kimebadilika sura. Hapo unaweza kukibonyeza na kuendelea kusoma kurasa uliotaka.
App hii ina tabia za app za ku-soma baadae kama Pocket. Kurasa zinafunguka na makala tu, bila mbwembwe zinazopunguza umakini wa usomaji.
Flynx siyo kivinjari kamili na huduma kama “copy and paste” utazikosa. Hii ni kwa sababu Flynx imetengenezwa kuokoa muda na kurahisisha maisha. Unapotaka kutumia chaguzo za kivinjari cha kawaida unaweza kufanya hivyo kirahisi. Fungua menu kwenye kiputo cha Flynx na chagua kivijari chako.
App hii ni moja ya app zinazosifiwa na mitandao maarufu ya teknolojia kama techrepublic, wired na androidcentral. Pengine ni muda wa wewe kujaribu Flynx au kivinjari chochote cha kuelea na tuambie imebadilishaje matumizi yako ya kuperuzi intaneti.
Angalia video ifuatayo kuona inavyofanya kazi.