Sio siri kuwa kampuni ya Google ilikua na mpango wa kutengenezea mfumo endeshaji ambao ni mbadala kwa Android. Ikumbukwe kuwa Android ndio mfumo wa uendeshaji ambao umezoeleka sana na umesambaa katika simu nyingi duniani kuliko mwingine wowote.
Jambo hili halikua siri sana kwani hata jina lako OS hiyo limewekwa wazi kuwa itaitwa Fuchsia ripoti zinasema kuwa Google wamekua wakiwa wakilifanya swala hili kwa kipindi cha muda mrefu tuu lakini hakukuwa na vithibitisho thabiti.
Mpaka sasa ni kwamba Kampuni imeweka katika mtandao baadhi ya taarifa za OS ya Fuchsia na pia wale wakosoaji na waboreshaji (developers) wamepewa uwezo wa kuweza kutumia Os hiyo na kutoa maoni yao katika mtandao.
Ma’developer wote wanaweza fuatilia OS hii kwa kuingia katika mtandao spesho unaujulikana kama Fuchsia.dev ili kuweza kuwasilisha mawazo yao kuhusiana na OS hiyo.
Ukiingia katika mtandao huo kuna taarifa mbalimbali na nyaraka ambazo zinahusu OS Fuchsia na pia mtandao huu utakuwa ni wa wazi kama vile ilivyo kwa upande wa Android.
Fuchsia itakua inapatikani katika vifaa vyote– kuanzia simu janja mpka kompyuta– Os hii, tangia mwishoni mwa mwaka 2016 imekua katika hatua za mwanzo mwanzo tena kwa siri lakini kwa sasa mambo yamebadilika na iko wazi katika macho ya watu.
Soma Zaidi Hapa Kuhusu Fuchsia