Kama ni mpitiaji mpitiaji mzuri kwenye mtandao basi pengine umekutana na habari hii ambayo pengini kwa kiasi kikubwa imewashtua wengi sana, teknolojia hii si nyingine ni EctoLife.
Kwa mara ya kwanza kabisa nilipata video inayoelezea namna teknolojia ya EctoLife inavyofanya kazi kupitia kundi la WhatsApp nikaona hii ni ya kuileta kabisa hapa TeknoKona.
Teknolojia hii kwa sasa ipo katika hatua za mwanzo kabisa na kazi yake kubwa ni kuwawezesha wazazi kutengeneza mtoto bila hata ya mama kubeba mimba kwa kutumia msaada wa fuko la uzazi la kiteknolojia.
Katika teknolojia kuna mambo ya kushangaza yaani mzazi anaweza akachagua jinsi anavyotaka mtoto wake awe vitu kama rangi ya ngozi, macho, nywele, urefu n.k wazazi wenyewe wanaweza wakapanga
Hii ni teknolojia ya kushangaza sana maana kwa tafsiri hii ni kwamba mtoto anatengezwa kiwandani kabisa yaani kama unavyoona simu inavyotengenezwa au kifaa chochote.
Ectolife sio kwamba imeshaanza kufanya kazi, la-ha-sha, kwa sasa ipo katika hatua ya WAZO tuu na tayari imeshapata mirejesho mingi sana.
Waliokuja na WAZO hili wanadai kuwa, kiwanda kitakua na maabara 75 zenye vifaa vya kutosha pia maabara hizo zitakua na mifiko bandia ya uzazi (Artificial Wombs) 400 na kwa mwaka mzima wanaweza tengeneza mpaka watoto 30,000.
Kuna wale ambao wanapongeza sana WAZO kama hili kwani linakuja kusaidia wengi hasa wale ambao wana matatizo katika mfumo wao wa uzazi mfano wale ambao wakishika mimba inaharibika😔
Ni wazi kwamba watu wana matatizo mengi sana ambayo pengine huenda wakalazimika kabisa katika kutumia teknolojia hii.
Kuna wale ambao wanapingana kabisa na WAZO hili huku wakiamini kabisa kazi ya kutengeneza kiumbw (mwanadamu) ni ya mungu kupitia kwa njia ambayo inafahamika ya kukutana kwa mwanamke na mwanaume.
Kuna wengine wamekua na mawazo tofauti tofauti juu ya WAZO hili ikiwemo na ile dhana ambayo wanahisi wanawake wengi watakimbia jukumu lao walilopewa na mungu – kuzaa kwa uchungu.
Kuna mwingine anaweza akaepuka kubeba mimba na kuzaa kwa uchungu tuu ili mradi tuu kuna teknolojia ya EctoLife.
Wewe una mawazo gani kuhusiana na WAZO hili? Hebu tiririka hapo chini katika eneo la comment, ningependa kusikia kutoka kwako.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.