Teknolojia Hii unaweza iita Underdisplay Fingerprint ila Kwa Apple twende na under display touch ID. hiki sio kitu kigeni kabisa maana simu nyingi tuu inatumia teknolojia hii.
Kinachotokea hapa ni kwamba hapo awali ‘Touch ID’ ilikua inafanikiwa maana teknolojia hii ilikua katika ‘Home button’ ya baadhi ya matoleo ya iphone.

Kumbuka sasa iPhone zinazokuja hakuna tena kitufe cha ‘home button’, hivyo basi uwezo wa sensa ya fingerprint haukuweza kufanikiwa katika ‘home button’ na pengine simu za iPhone za mwaka 2022 pengine zinaweza zikaitwa iPhone 14?
Hizi bado zinabaki kuwa kama fununu tuu maana hakuna vyanzo rasmi kutoka Apple ambavyo vimethibitisha jambo hili.
Kwa Apple kuja na teknolojia ya ‘under display fingerprint’ ni swala dogo kabisa maana kuna makubwa wameshafanya ukiachana na kwamba teknolojia hii ni ya kawadia sana.

No Comment! Be the first one.