Tuna mwaka tuu tupate toleo jipya –iPhone 15 — kabisa la iPhone sio? Ni mwezi wa tisa tuu mwaka 2023, lakini kuna fununu za kutosha tayari kuhusiana na simu hii.
Fununu zipo nyingi, lakini tugusie zile chache tuu ambazo tunadhani kweli zinaweza zikawa katika simu hii mpya ambayo tunaitegemea mwezi wa tisa mwaka huu.
USB TYPE-C
Hii tumeshaipigia kelele sana soma vizuri >>HAPA<< na hata >>HAPA<< ni wazi kuwa tuazidi kuona vifaa vingi sana vya kielektroniki ambavyo vitahamishwa na kuanza kutumia USB Type-C.
Hili lina hati hati kubwa sana ya kupatikana katika toleo lijalo la iPhone 15 itakayotoka mwaka 2023
Fahamu aina za USB >>Hapa<<
VIBONYEZO VISIVYOBONYEA – KATIKA SAUTI NA SEHEMU YA KUZIMA/KUWASHA/KULOKI SIMU
Mpaka sasa hakuna uhakika kabisa wa jambo hili lakini inategemewa kuwa kampuni ya Apple inaweza ikaja na iPhone 15 ambayo vibonyezo vyake vya pembeni ambavyo havibonyezeki.
Sasa unaweza ukawa unajiuliza vibonyezo hivyo vitakuaje? Lakini kama umeshawahi iona na kugusa kitufe cha nyumbani (home button) cha iPhone 7 basi itakua na mfumo huo pengine.
Ni lazima ukigusa hapo utapata mrejesho kwa njia ya ishara kwamba unafanya kitu fulani labda kuongeza au kupunguza sauti n.k.
UKUBWA SAWA
Katika swala zima la ukubwa wa vifaa hivi pengine inawezekana ikawa ni sawa tuu na hizi ambazo zipo kwa sasa kwa iPhone 14
DYNAMIC ISLAND KUWA KATIKA KILA TOLEO
Kipengele hiki ni kipya na kimeanza kupatikana katika baadhi ya iPhone 14, lakini katika matoleo ya iPhone 15 kitakua katika kila toleo.
Dynamic Island ni moja kati ya kipengele cha muhimu kabisa na kilichokonga nyoyo za wengi maana wemependezwa nacho, na kinatumiaka kama moja ya njia muhimu ya kuonyesha taarifa (notification) mbalimbali.
ONGEZEKO LA UJAZO UHIFADHI WA RAM
Kingine kinachotegemewa kwa hamu ni kwamba inasemekana kuwa toleo lijalo la iPhone litakua na ujazo uhifadhi wa RAM ambao ni mwingi ukilinganisha na matoleo ya nyuma
KUBADILIKA KWA JINA
Sio Jina la iPhone, la-ha-sha. Hapa nazungumzia kubadilika kwa matoleo makubwa, kwa sasa matoleo makubwa ya iPhone yanaitwa Pro Max.
Jina la Pro Max litaweza kubadilika na kuwa Ultra, pengine tegemea kuwa na toleo la iPhone 15 Ultra.
TEKNOLOJIA YA LENSI YA ‘PERISCOPE’ KATIKA KAMERA
Wakati baadhi ya simu katika Android ziliweza kupata teknolojia hii kwa muda tuu mpaka sasa, pengine Apple watakuaja nayo katika matoleo ya iPhone 15
Lensi ya Periscope kazi yake kubwa ni kuweza kuvuta (zoom) kwa umbali mrefu kuliko lensi za kawaida za telephoto ambazo zinatumika na simu janja nyingi.
CHIPU (CHIP) MPYA
Matoleo ya iPhone 15 kwa kiasi kikubwa sana zinaweza zikawa na chip mpya –3 Nanometer A17—na hii inatarajiwa kuongeza ufanisi wa simu zaidi na zaidi.
Ufanisi unaweza ukaongezeka zaidi ya asilimia 10 hadi 15 na vile vile hata kupunguza uwezo wa kupunguza nishati (chaji kuisha) kwa mpaka asilimia 30.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje? Katika hizo tulizondika unadhani ni zipi zin hati hati kubwa ya kuwepo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.