Katika dunia ya leo iliyotawaliwa na teknolojia si kitu cha ajabu ukisikia/kuona sifa za bidhaa fulani zikiwekwa hadharani japo kwa uchache lakini mtu au watu waliohusika kufanikisha hilo wana lengo lao basi ndio kilichotokea kwa rununu Google Pixel 4a.
Kwa wale tunaopenda kuperuzi huku na kule tukifuatilia habari za teknolojia basi sina shaka ulishakutana na dodosa za ujio wa Pixel 4a kwa maana ya kwamba sifa zake pamoja na mambo mengine. Kupitia picha jongefu iliyowekwa hivi karibuni kwenye Youtube imeweza kuweka wazi sifa muhimu za simu hiyo.
Fununu hiyo ilihusish vipengele ambavyo watumiaji wengi wa simu wanaviangalia kwa jicho la karibu na kuweza kufahamu kama itawafaa au la! Pata kufahamu yaliyofahamika mpaka hivi sasa kwenye toleo jipya kutoka familia ya Google Pixel:
Kipengele |
Uwezo |
Kioo | Inchi 5.81 (1080*2340px) |
Kipuri mama | Snapdragon 730 |
Kamera |
Nyuma: MP 12 (ina uwezo wa kuchukua picha mnato za ubora wa 4K) Mbele: MP 8 |
Diski uhifadhi | RAM: GB 6
Memori ya ndani: GB 64 |
Mengineyo |
Ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, USB Type C, betri lina uwezo wa 3080mAh, inatumia kadi mbili (2) za simu. |

Mbali na simu hiyo pia kuna majina matatu ambayo yanaaminika kutambulisha simu za toleo husika: Sunfish, Redfin na Bramble zikilenga Pixel 4a 4G, 4a 5G na 4a XL 5G ambazo hizo mbili za mwisho zinaaminika zitatumia Snapdragon 765 kwa ajili ya kuweza kuhimili kizazi cha tano cha kasi ya intaneti.
Hayo ndio machache ya muhimu ambayo wengi wetu ndio huwa tunatolea macho pale tunapotaka kununua simu janja. Hizo ni taarifa za awali na nina imani rununu husika itakapozinduliwa basi sifa zake zitakuwa zina shabiana na hizo nilizoziainisha hapo juu.
Vyanzo: GSMArena, Android Authority
One Comment
Comments are closed.