Huawei ni moja ya simu janja ambayo ina mafanikio makubwa sana hasa kwa nchi zenye watu wenye kipato kidogo. Kuna matoleo mengi sana ya simu hizo, kuanzia yake ya bei ya chini kabisa mpaka zile za juu.
Kwa sasa kampuni Huawei inategemea kuzindua simu yake ya huawei P9 ikifika mwezi wa nne mwaka huu. Fununu zilizopo ni kwamba mwezi huo kampuni hiyo itatangaza matoleo manne ya simu hiyo (Huawei P9) ambayo yatakuwa ni Huawei P9, Huawei P9 Max na Huawei P9 Lite.
Ripoti iliyopo ni kwamba raisi wa kampuni hiiyo ameonekana akitumia simu ya huawei yenye kamera mbili kwa nyuma ambayo inasemekana kuwa ni Huawei P9. Pia inasemekana kuwa matoleo yote ya Huawei P9 yatakuwa na kamera mbili (Dual-Camera) kwa nyuma.
Kwa wapenzi wa Huawei au hata wale wa picha wakae mkao wa kula kwa hili. Simu hiyo licha ya kuwa na kamera mbili za nyuma kwa ajili ya picha, bado kuna flash pembeni yake kwa ajili ya kutoa mwangaza katika kipindi cha giza. Pia katikati mwa simu hiyo kwa nyuma kuna sehemu spesheli kwa ajili ya sense ya kidole (fingerprint sensor).
Kwa kuwa Huawei watazindua simu hiyo mwezi wan ne tarehe 6 basi bila shaka wapenzi wa kampuni hiyo hawatasubiri sana ili kujionea simu janja hii.
Kampuni hiyo pia walitoa picha tatu ambazo zilikuwa na Hashtag ya #OO (kwa haraka hara hizi ni kamera mbili za nyuma za simu hiyo). Katika moja ya picha hizo imeonyesha ikiwa imepigwa ndani ya maji ambapo kulikuwa na mtu (mwogeleaji) akiwa karibia na mnyama wa majini maarufu kama ‘Dolphin’, sasa swali lililopo je simu hiyo itakuwa haiingia maji (waterproof)?. Jibu litapatikana mwezi wan ne tarehe 6 bila shaka.
Huawei P9 itakuwa na uwezo wa RAM wa GB 3 na uwezo wa uhifadhi wa GB 32 (ukija kabisa na simu hiyo).Huawei P9 Lite yenyewe itakuwa na uwezo wa RAM wa GB 2 na ujazo wa GB 16 (ukija nazo kabisa). Mwisho kabisa Huawei P9 Max itakuwa na uwezo wa RAM wa GB 4 na pia itakuwa na ujazo wa GB 64 ikiwa inakuja nazo kabisa.
Soko la simu janja linakuwa kwa kiasi kikubwa sana siku hizi kutokana na hilo makampuni ambayo yatengeneza simu hizi hasa makampuni yenye majina makubwa inawabidi wafanye juu chini ili mradi kuja na kitu ambacho hakipo sokoni na kitakacho wavutia wateja wao. Kwa kufanya hivyo wanaweza wakaliteka soko la simu janja.
Mauzo mengi ya simu kwa kampuni moja inaamaanisha mapato mengi kwa kampuni hiyo. Tumeona mapinduzi yaliyoletwa na kampuni la Apple, makampuni mengine hayana budi kuiga.
One Comment
Comments are closed.