Katika soko la magemu ni wazi kwamba Playstation ambao wanamilikiwa na kampuni ya Sony ndio kinara katika uwanja huo.
Fununu hizi za kifaa kingine cha Playstation kwa maana ya PS5 zilianza kuvuma mwaka 2020 miezi michache tuu baadha ya toleo la PS5 kuingia sokoni.
Kama umegundua siku hizi teknolojia nyingi zikiachia vifaa vyake huwa zinaachia toleo moja zaidi ya mara moja kwa mfano unaona kabisa hata iPhone 14 zilivyotoka zilitoka na zile zingine za iPhone 14 Pro.
Japokua mpaka sasa bado kampuni ya Sony wenyewe hawajaweka wazi kuhusiana na jambo hili –kwamba watafanya uzinduzi mwakani—lakini vyanzo mbalimbali vya kuaminika vinatoa taarifa hizo.
Ni wazi kwamba toleo lijalo litakua na maboresho kadha wa kadha katika hali ya kuhakikisha kuwa linajitofautisha kabisa na toleo la PS5 ambalo lipo katika soko.
Kingine ambacho kiliashiria kwamba kampuni hiyo inakuja na toleo hilo jingine ni pale kampuni ilipowasilisha ombi la hakimiliki nyingine ya PS5 ambazo ni tofauti na hizi ambazo zipo katika PS5 iliyopo sokoni
Sony Interactive Entertainment has filed a new patent that suggests the format holder is looking to optimise its ray tracing effects on #PS5
— Gamingnews (@Onion00048) February 25, 2022
kulingana na utaratibu ambao Playstation unao ni kwamba kuna hati hati kubwa toleo la PS5 Pro likatoka mwakani katika kipindi cha sikukuu…
… Hii ni kwa muenendo wao kumbuka toleo la PS4 lilitoka mwezi novemba 2013 na huku PS4 Pro ikitoka mwezi novemba mwaka 2016 ikiwa ni miaka mitatu baadae.
Playstation 5 ni moja kati ya matoleo ya PS ambayo yamepitia changamoto nyingi sana ikiwemo uhaba wa malighafi katika uzalishaji, uzalishaji mdogo na vile vile hata baadhi ya masoko kupandishiwa bei zaidi.
Soma kila kitu kuhusiana na PS5 >>>HAPA<<<
Mambo ni mengi wakati hatujamalizana na hili kuna vyanzo vingine pia vinasema kwamba matoelo ya PS6 yataanza kuingia sokoni rasmi ifikapo mwaka 2028!
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini hivi umeshawahi kutumia toleo la PS5 katika kucheza gemu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.