TECNO ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika maswala mazima ya kutengeneza na kuuza simu.
Kwa afrika TECNO inashikilia namba za juu kabisa kwa wale ambao wanaongoza kuuza simu kwa wingi, hii inamaanisha kidunia iko katika namba nzuri tuu.
Mara kwa mara kampuni imekua ikitoa simu kadha wa kadha ambazo kwa namna moja au nyingine zimekua zikileta mapinduzi ya kiteknolojia katika soko.
Kwa taarifa zilozopo sasa hivi ni kwamba kampuni iko katika hatua za mwisho kuachia simu yake ya kwanza ambayo itakua ni ya kujikunja (flip)
Simu hii itakwenda kwa jina la TECNO Phantom V Flip, hii inaamanisha kwamba huu ni muendelezo wa matoleo yale ya familia ya Phantom.
Simu hii mpaka sasa hakuna mtu ambae amaiona na kusema muonekano wake lakini kitu ambacho kimewapa watu picha ni baada ya kava la simu hii kuzunguka katika mtandao.
Awali kabisa kava hilo limeonekana katika soko la kimtandao huku likionyesha kwamba simu hiyo itakua na kioo kwa nyuma ambacho pengine kitakua ni kwa ajili ya taarifa (Notification)
Mpaka sasa sifa za undani za simu hii hazijulikani lakini kwa haraka haraka ni kwamba itakua na sifa za undani za hali ya juu maana matoleo yote ya phantom yanakuaga na sifa za ndani za juu kulingana na kipindi husika.
Baki nasi na tutakujuza juu ya sifa za undani pindi tuu TECNO wenyewe watakavyo zitangaza katika utambulisho.
Kingine ni kwamba tunategemea hata bei ya kifaa hiki itakua ni ya juu maana teknolojia inayotumika katika kutengeneza simu za Flip ni kubwa ukilinganisha na simu janja za kawaida.
Nignependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje unadhani ni sahihi kwa TECNO kuingia katika soko la Flip? Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.