Hizi habari zimesambaa sana kwamba kampuni nguli ya kiteknolojia yaani Apple ina mpango wa kuinunua Man U na hii ni mara tuu ya baada ya kusikia kwamba timu hiyo ya mpira iko sokoni.
Ukiachana na swala hili la timu kuuzwa bado timu ilikua inazungukwa na habari kadha wa kadha kubwa kabisa ilikua ni ile ambayo ilimfanya CR7 kuondoka Man U na hii ni kabla kabisa ya hii ya Apple.
Apple ni moja kati ya makampuni ambayo yana utajiri wa hali ya juu kabisa na kama ikiwa na nia dhahiri ya kuinunua Man U basi kwao watatoa hela ndogo sana.
Kwa sasa inasemekana kwamba Man U iko sokoni na thamani yake ni kiasi cha Euro Bilioni 5.8 huku vyanzo vingine vikiandika kwamba inaweza kufika mpaka 6.
Ikumbukwe kwamba kampuni ya Apple haijawahi kumiliki asilimia nyingi katika kampuni nyinigine yeyote ambayo inajihusisha na maswala ya michezo.
Man U ilitangazwa kuuzwa na wamiliki wake ambao wanamilikia asilimia nyingi sana, The Glazers ambao wamekua wakimiliki timu hiyo kwa zaidi ya miaka 17.
Nimesema Euro bilioni 6 ni ndiogo sana kwa Apple maana kwa mwaka tuu Apple huwa wanatengeneza faida mpaka ya Euro bilioni 326.
Watu waliojikita katika teknolojia na hata makampuni mengi kataka nyanja hii wamefanya manunuzi makubwa sana kwa kipindi cha hivi karibuni.
Soma Zaidi Bwana Elon Musk Kuinunua Twitter >>HAPA<<
Vyanzo vingine kama vile MacRumors vinakataa taarifa hii kwamba sio ya ukweli kwamba ni fununu tuu.
Vyanzo vinasema kuna viashiria vingi sana vinavyoonyesha kuwa Apple inaweza ikawa na mpango dhahiri kabisa wa kuinunua Man U na kwa hivi karibuni imeonekana ikianza kujiingiza katika michezo kidogo kidogo.
Tusubirie tuone kama itauzwa kwa kiasi hicho cha dola bilioni 7 za kimarekani na mmiliki mpya atakua ni nani baada ya familia ya Glazer kuuza.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni kama Apple kuingia katika biashara inayohusiana moja kwa moja na mpira?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.