Ni wazi kwamba Galaxy Z Flip 5 inasubiriwa kwa hamu kabisa na hii inategemewa kuwa ndio muendelezo wa Galaxy Z Flip 4 ambayo mpaka sasa ipo katika soko.
Inajulikana kwamba kampuni ya Samsung mara kwa mara inatengeneza simu kali sana za kujikunja na mpaka sasa kampuni hiyo ndio inshikilia usukani katika soko la simu za aina hii na mwaka huu ni zamu ya Galaxy Z Flip 5.
Kwa sasa kampuni inatamba na matoleo yake ya Galaxy Z Fold 4 na Galaxy Z Flip 4 lakini inaonekana dhahiri kwamba mwaka huu itakuja na matoleo ya juu zaidi .
Matoleo hayo ni Galaxy Z Flod 5 na Galaxy Z Flip 5, lakini kwa sasa tuongelee tuu kuhusiana na muonekano wa Galaxy Z Flip 5 ambao unaonekana katika baadhi ya mitandao.
Galaxy Z Flip 5 inaonekana ikiwa na mabadiliko makubwa sana –ya kimuoneknao—ukilinganisha na toleo lake la nyuma.
Kile kioo chake cha nyuma –kinachoonekana baada ya kuifunika—kimekua ni kikubwa zaidi na vile vile muonekano umebadilika.
Vyanzo vinasema kioo hicho kitakua na ukubwa wa inchi 3.4 wakati kioo cha ndani kikiwa na ukubwa wa inchi 6.7.
Ukubwa wote wa simu utakua katika vipimo vya 165mm X 71.8mm X 6.7mm ambapo kwa haraka haraka hii itakua na ukubwa kwa kila kitu ukilinganisha na ile ya mwanzo.
Kama una kumbukumbu nzuri mwanzoni tuu mwa mwaka huu kampuni ya Oppo ilizindua simu ya aina hii ambayo ilikua na kioo kikubwa cha nje (ukiwa ushaikunja) na watu wakapongeza sana hili. Simu hiyo inakwenda kwa jina la Oppo Find N2.
Kingine kikubwa katika simu hizi za kujikunja mara nyingi kampuni zinashindwa kuzifanya simu hizo zisiache nafasi kabisa katika kujikunja.. nyingi huwa zinaacha kauwazi Fulani hivi.
Pengine hili Samsung wameliona na wanalifanyia kazi katika matoleo haya yanayotarajiwa kutoka mwaka huu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katikwa uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Je ushawahi kutumia simu janja za aina hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.