Watu wengi duniani wanatumia simu janja zinazotumia Android (toleo la karibuni) na huwezi kuikuta ikawa haina programu tumishi kwa ajili ya kuhifadhi picha ambazo zinakuwa katika mpangilio maalum kulingana na vigezo mbalimbali.
Wale wote ambao tuna rununu (simu janja) tunafahamu fika mbali na kuwepo kwa kikasha cha picha (Gallery) lakini pia kuna mfuko mwingine ambao pia mewekwa mahususi kwa ajili ya kutunza picha jongefu, picha, n.k lakini kitu kikubwa ambacho pengine wengi wetu hatujawahi kuona kuwa ni kadhia pale linapokuja suala la ukubwa wa kitu chenyewe na ukweli usiopingika Google Photos inachukua MB 130 lakini sasa hivi karibuni mbadala wa Google Photos umeingia sokoni; unaitwa Gallery Go.
Je, Gallery Go ina sifa gani?
Sifa za Gallery Go hazitofauti sana ana zile za kwenye Google Photos kwa maana ya kwamba yale ambayo yanaweza kufanyika bila ya mtu kuyafanya mathalani kupanga vitu ambavyo vinahifadhiwa huko kulingaba na tarehe, faili pamoja na vigezo vingine kadhalika kitu ambacho inafanya programu tumishi husika iwe katika muonekano nadhifu ndani yake lakini utofauti mkubwa utaonekana kwenye mambo yafuatayo:-
- Gallery Go ina ukubwa wa MB 10 kulinganisha na MB 130 za Google Photos,
- Gallery Go inakubali kufanya kazi kwenye Android 8.1 (Oreo) au zaidi ya hapo ilihali Gogle Photos inakubali hata kwenye Android toleo ya zamani kidogo,
- Gallery Go ina uwezo wa kufanya kazi bila kuhitaji intaneti.
Gallery Go tayari inapatikana kwenye Playstore ingawa usijisumbue kuishusha iwapo simu janja haitumii Android 8.1 kwani chini ya hapo haitakubali kuhifadhiwa. Sisi ndio TeknoKona, usisite kutufuatilia kila uchwao.
Vyanzo: GSMArena, Android Police