Wengi wanaamini Afrika inaweza tengeneza mambo mengi ya kiteknolojia kama kukiwa na sapoti ya kutosha asa kwenye suala la pesa. Wote tunafahamu ya kwamba serikali zetu haziwekezi vya kutosha katika ubunifu na uzinduzi wa kiteknolojia na hakika watakupa sababu ya kwamba suala la bajeti linabana….bado tuna matatizo kwenye mahospitali na ata elimu hivyo huko ndiyo muhimu zaidi. Je ushawahi sikia kuhusu teknolojia ya gari lisolotumia mafuta?
Uganda wamejisogeza mbele zaidi kiteknolojia, wamefanikiwa kutengeneza gari linalotumia umeme na si mafuta la kwanza kabisa kwa Afrika. Teknolojia hii inakua zaidi nchi za ulaya na marekani lakini kwa Afrika Uganda imetuletea gari la kwanza kabisa.
Sikiliza mahojiano yaliyofanywa na BBC Swahili katika uzinduzi wa gari hilo jijini Nairobi.
No Comment! Be the first one.