Gmail ndio huduma inayotumia na watu wengi sana katika maswala ya barua pepe (email) na vile vile ina umaarufu mkubwa sana.
Mara kwa mara Gmail imekua ikifanya maboresho au kuongeza vipengele mbalimbali ili kuhakikisha inateka mioyo ya wateja wake.
Sasa hivi ni zamu ya App yake katika simu, na sasa huduma ya kutafsiri (translate) imkeuja katika App hiyo ya Gmail ya simu.
Zaidi ya lugha 100 zimeongezwa katika huduma hiyo ili kuhakikisha mtu anweza soma barua pepe (email) hizo katika lugha ambayo anaipendelea yeye.
App ya Gmail yenyewe itakuwezesha kuchagua lugha ambayo unataka kuitumia katika kusoma barua pepe zinazokuja na utaweza fanya hivyo kwa kuingia katika eneo la Settings na kufanya machaguo yako.
Unauwezo pia wa kuzima kipengele hiki ili kutumia Gmail kama ilivyokua mwanzo au pia unaweza ukafungua barua pepe husika na kisha ukaingia katika vile vimistati (vidoti) vitatu na kisha kuchagua lugha ambayo unataka kusomea barua pepe hiyo.
Uzuri wa jambo hili ni kwamba kuna hatihati kubwa kwamba katika pembe yeyote ya dunia ambayo upo ni lazima lugha moja (ambayo ni chimbuko) utakua unaijua kati ya hizo zaidi ya 100.
Kwa sasa kipengele hiki kimeanza kusambaa kwa watumia wa App katika Android na itachukua mpaka siku 15 kuwafikia watumiaji wote wa Android.
Kwa watumiaji wa iOS kipengele hiki kitaanza kupatikana katika App ya Gmail mpaka kufikia tarehe 21 agosti 2023 hivyo haina budi kusubiri.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment je unaonaje kuhusiana na jambo hili kutoka Gmail? Je utatumia kipengele hiki?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.