Gmail ni moja katika ya huduma za barua pepe ambayo ni maarufu kuliko zote maana ndio yenye watumaiji wengi Zaidi.
Google ilitangaza kubadiisha muonekano wa Gmail tangia mwezi januari mwaka huu, na toleo hilo likatoka lakini kwa baadhi ya watumiaji waliochaguliwa.
Sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Google kubadilisha muonekano wa baadhi ya huduma zake, sasa muonekano huu mpya utaonekana na utakuwa ukitumika na watumiaji wote ambao wamewasha huduma ya Google Chat

Kabla ya kuanza kufikiria mbali zaidi, subiri kwanza. Hapa huduma haijafanyiwa mabadiliko makubwa sana maana imejikita tu katika muonekano na mpangilio wa vitu.
Ni ishu ya muonekano tuu, na muonekano huu utasaidia kwa namna moja au nyingine huduma za Chat, Spaces, na Meet n.k ziweze kupatikana vizuri ndani ya huduma hiyo.
Kingine kizuri ni kwamba kama ukiwa hujapenda muonekano huo basi unaweza kurudia muonekano wa zamani, Hapa unaweza kwenda katika eneo la settings na kuingia katika “Go back to the original Gmail view,”
Ili kutumia huduma hii ni lazima uingie katika huduma hii ya barua pepe ya kwenye mtandao (kompyuta).

Ili kutumia huduma hii kama bado haijawezeshwa katika Gmail yako nenda katika eneo la Settings na kasha ingia katika upande wa Settings na kisha Try out the new Gmail view.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, Je umeshaanza kutumia huduma hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.