Chrome kutoka google ndio kivinjari (browser) ambacho ni maarufu sana na kina namba ya watu wengi ambao wanakitumia.
Kwa sasa Chrome ina Zaidi ya watumiaji bilioni mbili duniani kote na kutokana na kumbukizi hii ya 15 ya kunzishwa kwake google watangaza kuja na maboresho kadha wa kadha.
Kivinjari hiko kitapata mabadiliko kadhaa ya kimuonekano, na vile vile kutakua na vipengele vipya vya hapa na pale.
Muoneknao wa alama (icon) mbali mbali utabadilika na hata kutakua na rangi kadha wa kadha ambazo unaweza chagua ili kubadilisha muonekano.
Wengi wanadai Chrome ni moja kati ya vivinjari vikubwa na pendwa kwa sababu utumiaji wake una urahisi na pia kipo haraka wakati unakitumia.
Ni wazi kabisa kwamba katika kipindi cha hivi karibuni Chrome ya kompyuta itapata muonekano mpya kabisa na hata ‘Tabs’ na ‘Toolbar’ zinaweza kubadilika/kubadilishwa.
Ni wazi kwamba muonekano huu mpya lazima utakua unaendana na muonekano ambao Google wenyewe ndio wanautaka.
Ni wazi kwamba vitu vingi vya Google vina tabia ya kufanana haswa katika rangi na katika jambo hili itatumia teknolojia ambayo wanaiita “Material You Design Language”
Material You, ni mfumo ambao unasaidia sana katika swala zima la kuchagua rangi na hii inafanyika kwa hali ya kwamba mfumo mzima utachagua rangi kulingana na picha ya ‘Wallpaper’ ambayo umeiweka— mfumo huu kwa mara ya kwanza kabisa ulianza kutumika katika kwenye Android 12.
Ni wazi kwamba kwa muonekano huu mpya Chrome kabisa itabadilika na kuakisi ukisasa kabisa na kuleta mapinduzi makubwa ya vivinjari.
Kingine kikubwa ni kwamba muonekano huu mpya utakua na faida nyingi moja wapo ni hata kuwasaidia watu wenye matatizo ya macho kuweza kuona/kusoma vizuri wakati wakiwa wanatumia kivinjari hicho.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani muonekano mpya utakua na tija kwa watumiaji wa kivinjari hicho? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.