Kuna ‘browsers’ nyingi duniani ila zote zinalengo moja kuu, kukusaidia kutumia mtandao kwa uraisi zaidi hasa kwa kuzingatia kasi na ulinzi wa data zako.
Nadhani kwa wengi wetu Firefox na Internet Explorer ndio maarufu zaidi, hasa kama auna utundu wa kujaribu vitu vipya. Mimi natumia Ubuntu/Linux kwenye laptop yangu nayo kwa kuanzia huwa inakuwa ihsawekwa browser moja, nayo ni Firefox, kwa watumiaji wa Windows ni IE(Internet Explorer) ndo huwa inakuja nayo. Mimi nimekuwa mtumiaji mzuri wa Google Chrome, kuna vitu vyake mbali mbali (features) zinanivutia sana, lakini mara nyingi huwa natumia Firefox pia.
Source: StatCounter Global Stats – Browser Market Share
IE imekuwa inatawala asilimia kubwa ya browsers zote zitumiwawo duniani kwa muda mrefu sana, lakini sasa kuna habari nzuri, IE siyo baunsa pekee kwa sasa. Kuanzia mwanzo wa mwaka jana Google Chrome itengenezwayo na kampuni ya Google imekuja juu na mwezi huu kufanikiwa kuipiku IE kwa mara ya kwanza. Hakuna Web Browser nyingine yeyote iliyowahi kuotoa IE katika kuwa namba moja katika kutumiwa lakini Google Chrome imeweza.
Lakini kitu kilichonivutia zaidi ni kwamba kwa Tanzania utumiaji wa IE umeshuka na sasa ni Firefox ndo tunayotumia zaidi. Katika grafu kama inavyoonekana hapa chini, kwa mwaka huu inaonesha utumiaji wa Firefox umekuwa mkubwa kiasi cha kuipita IE lakini bado Google Chrome haifanyi vizuri sana, lakini sio mbaya, kwani naamini Google Chrome na Firefox ndo browsers nzuri zaidi.
Source: StatCounter Global Stats – Browser Market Share
Kwa Tanzania tunaona ukuaji wa Firefox na Google Chrome unazidi kuididimiza IE. Je wewe unasemaje? Unapendelea Browser gani zaidi?
No Comment! Be the first one.