Kwa miaka kadhaa sasa Google wamekuwa wakitoa bidhaa ambazo zinalenga kusaidia/kurahisisha upatikanaji wa vitu mbalimbali bila shida yoyote kwa mtoto aliye masomoni.
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya teknolojia utakuwa unafahamu kuhusu “Google Classroom” ambayo kwa sasa imeboreshwa ikiwapa nguvu zaidi walimu kuhakikisha mwanafunzi anatumia akili yake mwenyewe kuweza kufanya vizuri katika masono yake.
Google Classroom ni nini?
Google Classroom ilianzishwa mwezi Agosti, 12 2014 ambapo ni programu tumishi/tovuti (darasa) unaomuwezesha mwalimu kuwasiliana na wanafunzi wake/kuweka mazoezi, maandiko ya kujisomea na hata kuweka alama alizopata mwanfunzi.
Teknolojia hii inasaidia kupunguza matumizi ya kaalmu na karatasi na badala yake unatumia kompyuta/simu kupitia kivinjari au programu tumishi kuweza kukamilisha kazi.
Sasa katika masasisho mapya yaliwekwa kwenye programu hiyo imewaongezea uwezo walimu/wazazi kuweza kuzima programu tumishi/vivinjari wakati ambao mwanafunzi anapaswa awe amelala au anapotakiwa kuelekeza akili kwenye masomo yake.
Vilevile, mwalimu pia ana uwezo wa kuzuia mwanafunzi asiweze kutumia intaneti kuweza kutafuta majibu ya maswali wakati ambapo anafanya mazoezi jambo ambalo linamfanya mwanafunzi atumie akili yake tu kuweza kufanikiwa (kupata majibu ya maswali aliyoulizwa).
Darasa huru (Google Classroom). Utahitaji muda wako, kifaa cha kijiti kilichounganishwa na intaneti kuweza kuwa tayari kwa darasa.
Kutokana na ukuaji wa teknolojia pamoja na utandawazi imekuwa ni changamoto kuweza kufanikisha mwanafunzi asiweze kuibia lakini kwa hiki ambacho Google wamekiboresha inavutia.
Kama mtoto wako anatumia Google Classroom hakikisha haachi bali anaendelee kuitumia kila siku kwani itamsaidia. Wewe je, una mawazo gani?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
One Comment
Comments are closed.