Imegundulika kwamba mwaka 2014 kampuni ya Apple ilipokea malipo yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni moja, inaelezwa kwamba yalilipwa baada ya Apple kuiweka search bar ya Google katika iOS.
Katika taarifa iliyochapishwa na jarida la Bloomberg jarida hilo linasema kwamba taarifa hii imepatikana katika moja ya mafaili ya kesi inayoendelea kati ya Google na Oracle Corp ambayo ni kesi ya hatimiliki. Moja ya nakala laini za mafaili ya kesi hiyo ambayo yaliwekwa kupatikana kwa umma ilikuwa na taarifa juu ya malipo hayo. Hata hivyo baada ya muda nakala ya faili hili ambalo mwanzo lilikuwa linapatikana kwa uma liliondolewa (pengine ni baada ya Google kuomba litolewe).
Pengine unawaza kwanini habari hii imepata nafasi katika vyombo vya habari ulimwenguni…
- Kwanza ni muda mrefu kume kuwa na tetesi za kwamba Google wanawalipa Apple ili huduma yao ya utafutaji itumike katika ‘search bar’ ya kwenye iOS lakini tetesi hizi hazikuwahi kufikia level ya kuwa na ushahidi kama uliopo sasa. Hii imeifanya habari hii kuwa ndiyo ya kwanza kutoa na ushahidi wa kiasi ambacho makampuni haya hasimu yanalipana.
- Sababu nyingine inafanya hii habari ipate kiki kubwa ni ukweli kwamba Tim cook Mkurugenzi mtendaji wa Apple amekuwa ndiye mkosoaji juu ya jinsi Google wanavyo tumia data kutoka katika utumiaji wa huduma ya utafutaji (search) na kuzitumia hizo katika matangazo kumbe nyuma ya pazia kampuni yake imekuwa inatengeneza kiwango kikubwa cha pesa kupitia njia ambayo yeye anaipinga.
Kiasi hicho cha dola za kimarekani bilioni moja ni kiasi kikubwa na kibongo bongo kingeweza kujenga barabara karibu kumi kila moja ikiwa na urefu wa kama kilomita 400.
Malipo haya ya dola za kimarekani bilioni moja ni asilimia 34 ya mapato ambayo google inayapata kwa kuweka search bar yake katika vifaa vya Apple, hii inatoa picha ni kwa kiasi gani biashara ya utafutaji (search) ilivyo na pesa nyingi.
Endelea kufuatilia mtandao wako wa TEKNOKONA kwa taarifa mbalibali za teknolojia katika lugha yetu tamu ya kiswahili, Tuandikie mawazo maswali ama maoni nasi tutajibu.
No Comment! Be the first one.