Unakumbuka kipindi ugonjwa wa uviko ulivyopamba moto makampuni mengi yalibadilisha mfumo wa uendeshaji kabisa hata google ilikua hivyo hivyo.
Makampuni mengi ya kiteknolojia kama vile Google, yalipunguza sana wafanya kazi na kuhakikisha mlolongo wa kazi unapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Kumbuka kwa haraka haraka Google ilibadilisha kabisa mfumo mzima wa wataalam wanaofanyia katika vitengo vya Pixel, Nest na hata Fitbit.
Licha ya haya yote kufanyika bado kampuni imetoa taarifa kwamba imefikia muafaka wa kauchana na maelfu ya wafanya kazi katika vitengo tofauti tofauti ndani ya kampuni hiyo.
Wao google wanasema maamuzi hayo yamefanyika katika kuhakikisha kuwa kampuni itafanya kazi kwa ufanisi zaidi na kwa mazingira ya kazi yaliyo bora zaidi.
Mara nyingi makampuni haya ya kiteknolojia yanapitia changamoto hii ya kupunguza wafanya kazi nah ii inakua na sababu nyingi ikiwemo hata ukuaji wa teknolojia kwa ujumla.
Kampuni ambayo ni kampuni mama kwa Google inajulikana kama Alphabet ambayo mpaka kufikia mwezi septemba mwaka 2023 ilikua tayari imesha ajiri wafanya kazi 182,381.
Ningependakusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani Google iko sawa kwa kupunguza wafanya kazi hao?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.