Google licha ya kuwa ndio mtandao namba moja unaotembelewa duniani, chini ya kapeti kuna mambo mengi yanafanywa na kampuni hiyo ili kuhakikisha kuwa wanabakia kuwa namba moja.
Kuna kipindi tuliandika kuhusiana na Google kuwalipa Apple mamilioni ya dola ilimradi kuhakikisha tuu wenyewe ndio wanakua chaguo la kwanza (default) la ulazima katika matafufo katika kivinjari cha safari.
Ukiachana na Apple hata Samsung nao wameingia katika mchakato huo ambapo wenyewe wameingina katika dili ya miaka zaidi 4 na Google.
Kinachofanyika hapa ni kwamba search engine, voice assistant na Play Store zitakuja moja kwa moja katika vifaa vya Samsung.
Kingine cha kuzingatia hapa ni kwamba sio kwa Apple na Samsung tuu, ni wazi kwamba Google imeingia katika dili la namna hii na makampuni mengine mengi tuu ili kujihakikishia nafasi yake.
Kwa nafasi kubwa sana makampuni mengi ya kiteknolojia huwa yanafanya kazi kwa kuingia katika mikataba na kulipana ili kufanikisha biashara hiyo.
Makampuni yanaweza yakawa ni washindani wakuu lakini nyuma ya pazia wanauziana vitu vingi hata ambavyo vinawafanya wawe washindani.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ulikua unaijua hii? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment jinsi ulivyo ipokea!
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
Amazing Content Good Creativity Congratulations and keep it up…
Thank you.