Gmail ni moja kati ya jukwaa kubwa kabisa ambalo linahusisha na maswala mazima ya barua pepe na lenye watumiaji wengi kuliko wote.
Gmail kila kukicha inahakikisha kuwa inawaletea watumiaji wake vipengele vingi na huduma mpya ili mradi kuhakikisha kuwa wanapata kile kilichobora.
Kwa watumiaji wa mitandao ambayo inamilikiwa na Meta kama vile WhatsApp na Facebook inaweza ikawa sio kitu cha kushangaza maana vipengele hivyo vinapatikana katika mitandao hiyo.
Kwanza kabisa mwezi uliopita kulikua na fununu kwamba kuna kipengele hiki kinakuja kutoka Google na sio kingine ni Emoji Reaction
Kumbuka kwa kipindi cha nyuma kulikua na emoji za kawaida kabisa lakini kwa sasa kipengele hiko kimeshindiliwa nyama kidogo.
Kipepengele hiki kinatoka kwanza kwa watumiaji wa Android na kasha kitakuja katika iOS na vile vile katika Gmail ya mtandao.
Kipengele hiki ni kwamba hakina utaofauti mkubwa sana katika kutumiwa na vile kinavyotumiwa katika mitandao mingine ya kijamii.
Kwa sasa kipengele hiki bado kinaendelea kifanyiwa maboresho ili kuwa bora Zaidi, kwa sasa kinaendelea kutumiwa kama kawaida.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je kwa ujio wa kipengele hiki je kutakua na ulazima wa kujibu barua pepe kwa maneno au unaweza kujibu na emoji reactions tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.