Ni wazi kwa sasa akili bandia (AI) zipo za aina nyingi sana katika kampuni ya Google na nyingi zinafanya mambo mbalimbali kulingana na vile zilivyoamuriwa.
Teknolojia inakuwa kwa kasi sana na kila siku makampuni na watu mbalimbali hujikita katika kuhakikisha kuwa wanakuja na teknolojia mpya Zaidi au kuiboresha ile ambayo ipo mfano Google.
Akili bandia (AI) hii ambayo Google wana mpango wa kuja nayo itakusaidia kwa kiasi kikubwa kwa maswali ambayo unajiuliza mwenyewe mara kwa mara.
Hii inaonyesha kwamba unaweza ukawa na jambo lako pengine likawa linakutatiza kabisa baada ya kuongea na mtu mwingine kwa bahati ukaongea na Google na likapata ufumbuzi.
Kitakachofanyika hapa ni kwamba teknolojia ya AI itakua ikichambua Zaidi ya mambo 21 ya kitaalam nay a kibinadamu ambayo yanahusisha ushauri wa maidha, mawazo, kanuni za kupangilia vitu mafunzo n.k ili kuhakikisha kwamba watu watapata majibu mazuri.
Kwa hali hii unaweza hata uliza Google kwamba umuambia nini rafiki yako ambaye hukuhudhuria msimba wa nduguye na ikakupa majibu sahihi kabisa.
Majibu ambayo yatakua yanatolewa katika mfumo huu yataka yakitegemea sana na hali halisi ya wakati huo maana hayatakua yakifanana.
Wenyewe wanaita “personal life coach’ kwa tafsiri ya haraka haraka ni kama kocha/muongozi wa maisha binafsi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je unahisi teknolojia hii ikianza kutumika itakua ni msaada mkubwa kwa watu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.