Simu janja nyingi ziku hizi zinakuja zikiwa na saa janja zake na hilo linafanyika hata kwa saa janja za Pixel Watch ambazo nazo zina saa zake.
Mpaka sasa kuna matoleo mawili tuu yaani Pixel watch 1 na Pixel watch 2. Kutoka na chanzo cha kuaminika kinasema kuwa kampuni imepanga kuja na matoleo mawili ya saa hizo
Yaani katika toleo la Pixel 3 saajanja zitakua ni mbili na kwa haraka haraka ni kwamba zitakua zinapishana vipengele pengine na muonekano.
Kampuni inaenda kufanya jambo hili baada ya kupokea malalamiko kwa kipindi cha muda mrefu na malalamiko hayo mengi yakiwa ni kwamba saa janja hiyo ina umbo dogo.
Kwa Pixel 1 na Pixel two ilikua ni vigumu sana kujua tofauti zao mpaka uzigeuze kwa nyuma ndio utagundua tuu zina maumbile tofauti lakini kila kitu kipo sawa katika muonekano.
Kumbuka makampuni mengine kama vile Apple wenyewe wana matoleo ya saa janja aina mbalimbali yaani yenye maumbo madogo na zingine za maumbo makubwa.
Hili ni jambo zuri sana kama kampuni ya Google itakua imeliona hili na kuwaletea wateja wake toleo kubwa zaidi hii itaonyesha ni kwa kiasi gani inawajali.
Kumbuka toleo la Google Pixel Watch 2 lilitoka mwaka 2023 mwezi oktoba japokuwa toleo la saa halikufanya vizuri sana katika soko lakini toleo la simu lilifanya vizuri sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani toleo hili kubwa la saa hizo litakua ni mshindani mkubwa kwa saa janja za Apple na Samsung?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.