Licha ya kampuni kuwa kubwa sana katika maswala ya teknolojia, sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Google kuwa na kesi kama hizi na kulipa watu fidia.
Mwaka 2017, walipata kesi kuwa inawalipa kidogo mainjinia wake wa kike ukilinganisha na wale wa kiume, kesi ambayo iliwaladhimu walipe mamilioni ya dola.
Kwa sasa kesi iliyopo ni kwamba hata katika malipo ya vibarua bado google inawapendelea wanaume tuu huku kama kawaida wanawake wanabaguliwa.
Kesi hii inahisisha wanawake 15,500 ambapo kwa ujumla inabidi Google ilipe kiasi cha dola milioni 118.
Mara kwa mara Google imekua ikipata shida katika gepu lake kubwa la malipo katika ya wanawake na wanaume.
Hii inapelekea kampuni hiyo iaanze kufanya taratibu za kuwa na mchumi anaejitegemea ambae ataweza kufuatilia na kubaini gepu hilo na kuweka usawa wa malipo kwa wafanya kazi wote.
CHANZO: THE VERGE
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii umeipokeaje kutoka Google?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.