Baada ya ushindani wa muda mrefu kampuni ya Google yaamua kuua ushindani huo kwa kumwaga mabilioni ya dola kununua kampuni za Apple na Samsung. Na maamuzi ya haraka waliyoyaweka ni pamoja na kushusha bei za Samsung Galaxy S7 na zile za iPhone 6S kwa zaidi ya asilimia 60%.
ANGALIZO: HABARI HII ILIANDIKWA KAMA UTANI WA TAREHE 1 MWEZI WA NNE, 2016… Si ya kweli! 🙂
Google wametangaza ununuaji wa makampuni hayo makubwa duniani huku wakiahidi maboresho makubwa kuwa njiani. Hii ni pamoja na kuhamisha makao makuu ya Samsung kutoka nchini Korea Kusini na kuyahamishia nchini Marekani.
- Bei ya simu kutoka Samsung na Apple kushushwa kwa zaidi ya asilimia 60%
- Makao makuu ya Samsung kuhamishiwa Marekani
- Google wametumia zaidi ya asilimia 70% ya utajiri wao wote kuweza kufanikisha ununuzi wa kampuni hizi kubwa
- Ushindani katika soko la simu utakuwa mkubwa sana na inawezekana kampuni kama Tecno na Huawei zikapotea kabisa, kwani simu za iPhone na Samsung zitakuwa bei rahisi sana
- Watu wengi ambao hawajawahi kumiliki iPhone au simu za Samsung Galaxy wataweza kumiliki kwa mara ya kwanza
Tutazidi kukuletea habari zaidi kuhusu dili hili, je wewe umechukuliaje uamuzi huu wa Google?
Chanzo: Tarehe Mosi April | Angalizo: ni utani tuu :-) 1/04/2016