Kama wewe ni mfuatiaji mzuri wa Teknolojia hasa zile za makampuni makubwa huwezi liacha kampuni kubwa, Google. Na tukizungumzia kampuni ya Google ukiachana na teknolojia zake zingine ipo hii ya kuvutia kuhusiana na gari inayojiendesha bila dereva kuwa nyuma ya usukani.
Sawa tumesikia mengi ya ajabu kama vile gari isiyotumia mafuta n.k lakini hii ni ya ajabu zaidi ila kwa teknolojia ya kisasa ni jambo linalowezekana.

Najua kuna maswali mengi unaweza kujiuliza je ni vipi gari inafanya kazi (kuweza kujiendesha yenyewe) ukiwa na swali hilo hilo kumbuka pia teknolojia inakua kwa kasi sana. Google ni moja kati ya makampuni machache duniani yaliyo juu katika maswali ya ubunifu katika nyanja ya Teknolojia.
Google ilisema katika makala kwenye blog kuwa ajali zilizotokea kwa magari ya teknolojia hiyo ni tuu katika kipindi cha miaka sita (6). Ajali zote zilizotokea ni ndogo ndogo na zinazo pelekea taa kuvunjika. katika blog mwendeshaji wa programu ya gari zinazojiendesha zenyewe wa Google, Chris Urmson alisema kuwa Ajali huwa zinatokea kwenye gari wakati gari inaendeshwa na dereva mwingine wakati inajiendesha yenyewe.
Makala ya Urmson ilitoka siku moja na ripoti ya Associated Press (AP) ikiwa inaripoti kuwa magari manne (4) ya kujiendesha yenyewe yameonekana katika ajali California tangia mwezi septemba. Tatu kati ya hizo ni magari ya kujiendesha yenyewe toka Google na gari lingine ni lile linalomilikiwa na Delphi, kampuni kubwa inayosambaza magari.
Magari ya kujiendesha yenyewe kutoka Google yanafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza kabisa California na Nevada.
Angalia Video Ifuatayo Kufahamu Zaidi Kuhusu Gari Hizi Kutoka Google

No Comment! Be the first one.