Umoja wa Ulaya (EU) wataka Google na Facebook kuwekea alama taarifa, picha au video zinazotengenezwa na teknolojia ya akili bandia.
Teknolojia ya akili bandia (AI – Artificial Intellegence), inakua kwa kasi na sasa imefikia hatua ambayo ni vigumu sana kutofautisha kati ya picha au video ya kweli na zile zinazotengenezwa na mifumo ya AI.

Umoja wa Ulaya unaona kama sehemu ya kudhibiti vita ya taarifa mtandaoni inayoendelea kati ya Urusi na nchi rafiki za Ukraine – vita ya taarifa inahusisha watu kutengeneza picha au video zinazotengeneza habari/taarifa ambazo hazina ukweli na hali inayoendelea katika vita kati ya Ukraine na Urusi. Lengo linakuwa kuleta wasiwasi kwa wanajeshi wa upinzani au kubadili mtazamo au uelewa wa mambo kwa wananchi wa kawaida.
Makampuni makubwa ya kiteknolojia hasa yenye tovuti za mitandao ya kijamii inayotumiwa na watu katika bara hilo wametakiwa kuwa na teknolojia zitakazoweza kutambua na kuwekea alama kitu chochote kitakachowekwa kwenye mitandao hiyo ambacho kimetengenezwa na AI. Changamoto kubwa wanayokutana nayo ni kwamba kila teknolojia ya AI inavyozidi kukua ndivyo inavyozidi kuwa vigumu zaidi kutambua.
Tunakuacha na picha kadhaa ambazo si za watu halisi waliowahi kuishi, hizi picha zimetengenezwa na AI. Tovuti ya ThisPersonDoesntExist.com, yaani MtuHuyuHayupo, inatengeneza picha mpya kila ukiitembelea. Hizi picha zinazotengenezwa kwa AI zinapatikana kwa malipo.
Mfano huu unaonesha ni jinsi gani AI imeweza kutengeneza sura moja katika aina 3 tofauti za kiasili: Muafrika, Muasia na Mzungu
No Comment! Be the first one.