Je unafahamu Google na Microsoft wanatumia umeme mwingi kuliko ata Tanzania? Teknolojia imebadilisha maisha yetu kwa njia nyingi, lakini inakuja na gharama zake. Makampuni makubwa ya teknolojia kama Google na Microsoft hutumia umeme mwingi kuendesha vituo vyao vya data, ambavyo vinaendesha huduma zote tunazozipenda mtandaoni.
Utumiaji Mkubwa wa Umeme
Utafiti mpya unaonesha kuwa Google na Microsoft kila moja hutumia umeme wa terawati 24 (TWh) kwa mwaka. Hii ni sawa na matumizi ya umeme ya nchi zaidi ya 100, ikiwemo Iceland, Ghana, na ata Tanzania!
Utumiaji wa umeme wa Tanzania kwa mwaka
Ingawa matumizi haya ya Google na Microsoft ni makubwa, ni muhimu kuzingatia muktadha wa Tanzania. Nchi yetu kwa sasa inakadiriwa kutumia kiasi cha 10.34 TWh kwa mwaka (Chanzo – AFDB). Hii ina maana kwamba Google na Microsoft hutumia zaidi ya mara mbili ya umeme tunaotumia hapa Tanzania!
Athari kwa Mazingira
Matumizi haya makubwa ya umeme yana maana kwamba makampuni haya yanaathiri mazingira kwa kiasi kikubwa. Vituo vya data hutumia umeme mwingi kuendesha seva na vifaa vingine vinavyozalisha joto. Ili kupoza vifaa hivi, hutumia mifumo ya baridi ambayo nayo hutumia umeme zaidi.
No Comment! Be the first one.