Google News yabadilishwa muonekano wake katika ule muonekano wa kwanza katika kompyuta
Google News ni jukwaa kubwa la kupata habari za kimataifa na kitaifa ambazo zinagusa Nyanja mbali mbali.

Hapa Google inachofanya ni kutafuta habari kupitia vyanzo mbalimbali na kuziweka katika uwanja mmoja ambapo mtumiaji anaweza kuwa na uwezo wa kuzipitia zote hapo.
Sasa muonekano huu mpya umebadilika na muonekano mpya unaonyesha vipengele vya mwanzo mwanzo kuwa muhtasari kwa ajili yako, habari za ndani na zile ambazo mtandao umekuchagulia kwa ajili yako.
Hili limebadilika kwa kiasi kikubwa sana kwani kwa mara ya kwanza muonekano wake ulikua kama picha ya chini hapo inavyoonyesha.

Muonekano huu umebadilika kwa sasa na ikiwa ni kama njia ya mtandoa huo kujibiresha kimuonekano ili kuendnaa na kasi ya sasa jinsi ilivyo.
Vile vile kama mpangilio huo hujafurahishwa nao bado una uwezo mkubwa wa kuubadilisha muoneknao huo kwa kupangilia jinsi unavyotaka wewe mwenyewe.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini kwenye eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je huwa unatumiga Google News??
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.