Update mpya ya Google photos sasa itaweza kuruhusu mtu kuchagua kufuta nakala ya picha ambazo zimekwisha hifadhiwa katika mtandao, hii ina maana kwamba pindi app(kitumizi) hiki inapofanyia backup picha zako itafuta zile nakala halisi zilizo katika simu yako na hivyo kukupa nafasi katika simu yako kwa ajili ya mambo mengine.
Kama ni mtumiaji wa simu janja basi utakuwa unaelewa kwamba picha ni moja ya vitu vinajaza memory ya simu zetu, hatuwezi kukwepa kupiga picha ama hatuwezi kukwepa kupokea picha kutoka kwa rafiki na makundi yetu huko whatsapp maana haya ndio hasa sababu tunamiliki simu janja.
Google photos inataka tuzihifadhi picha zetu kwa kuzi upload (pandisha) katika hifadhi zao na kisha tufute nakala za hizo picha ambazo bado zipo katika simu zetu ili pindi tunapohitaji picha zile basi tuzishushe kutoka katika mtandao.
Update hii mpya ya Google Photos itakuwa na kitufe ambapo mtumiaji atachagua kufuta nakala halisi za picha zake ambazo zimehifadhiwa katika mtandao, chaguo hilo litamruhusu mtu huyu kuweza kufanya maamuzi kama anataka ama hataki kutumia huduma hii.
Ubaya ni kwamba kama utakubali kufuta nakala za picha zilizo katika simu yako ambazo zimehifadhiwa na google photos basi pindi pale utakapohitaji kuziona tena utahitaji kuwa na bundle.Hii ni huduma nzuri ila sio kwa kila mtu bali wale ambao wao hawatajari kutumia bundle kushusha picha zao pindi wanazihitaji.
Uzuri wake ni kwamba huduma hii itatuondolea ile kazi ya kufuta picha ambazo zimo katika simu zetu lakini hatuna matumizi nazo mfano picha tunazotumiwa katika mtandao wa whatsapp.
One Comment