Ni wazi kwamba vifaa vinavyotumia chapa ya Google Pixel vinafanya vizuri sana katika soko kwa sasa, moja kati ya vifaa hivyo ni simu za Pixel.
Kwa sasa kuna toleo la Google Pixel 7 ambazo zimefanya vizuri sana katika soko, vile vile chapa hiyo ina mpaka saa janja ambayo tayari iko sokoni.
Kwa sasa Google kupitia chapa hiyo hiyo ya Pixel inakuja na tabiti ambayo inakua ni toleo la mbele zaidi ya toleo ambalo kwa sasa lipo katika soko.
Kwa taarifa ambazo zipo ni kwamba hata bei ya tabiti hii itakua ni bei ya juu ukilinganisha na toleo la kwanza na itakua ni mshindani mkubwa sana kwa tabiti zingine ambazo zitakua katika soko.
Kwa sasa makampuni mengi huwa yanafanya juu chini katika kuhakikisha kuwa inawapatia wateja wake vifaa vya kielektroniki ambavyo ni bora na vizuri zaidi.
Vyanzo mbalimbali vinadai kuwa matarajio yao ni kwamba lazima tabiti hizo zitakua za aina yake nah ii yote ni kulingana na kwamba chapa ya Pixel huwa inatoa bidhaa za aina yake.
Licha ya yote haya kusambaa katika mitandao kwamba pengine Google ndio watakua wakifanya juu chini kwa sasa ili kuhakikisha wanazalisha tabiti hizi lakini wao hawajaweka wazi taarifa hizi.
Licha ya fununu hata sifa za undani za tabiti hii haziko wazi pengine ni mpaka tusubiri kampuni ya Google yenyewe ndio itoe sifa za undani kabisa za tabiti hizi.
Soma kila kitu kuhusiana na Google Pixel >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je unadhani tabiti hizo zitakua na ushindani mkubwa kwa tabiti zingine ambazo zimeshaliteka soko kama iPad?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.