Google iko katika mchakato wa kuachana na Google Play Movie & TV na kuenda katika kingine kabisa na hii ni wazi kabisa inaonyesha kwamba wanahamia kwingine.
Mpaka sasa Google wamepeleka wayeja wa Android na iOS katika App ya Google TV ambayo moja kwa moja ndio mbadala wa Google Play Movies & TV.
Kumbuka jambo hili limeanza kutekelezeka muda kidogo na sio kama linaaza sasa kwa mfano App hiyo iliondolewa katika huduma za Roku.
Fikiria katika Android TV huduma hii imetolea mwezi oktoba na kingine ni kwamba imeondolea katika TV janja (smart TV) nyingi tuu.
Lakini kingine ni kwamba kwa wale ambao bado wanapata huduma ya Google Play Movies & TV ni kwamba huduma hiyo mpaka kufikia januari itakua haipatikani kabisa.
Lakini Goolge itakua na namba ambayo unaweza kuangalia matazamo yako ambayo pengine uliyalipia kupitia huduma hiyo kabla ya kufungwa.
Kwa haraka haraka hapa hakuna kikubwa ambacho kimebadilika zaidi ya eneo ambalo utakuwa na uwezo wa kuangalia matazamo hayo.
Na kinachoonekana ni kwamba Google wanafanya haraka haraka ili kuhakikisha watu wanahamia katika huduma mpya kwa haraka iwezekananvyo ili maisha mengine yaendelee.
Ni kawaida kabisa kwa majukwaa kama haya kufanya maboresho na kuhamisha huduma zake kwenda katika jukwaa jipya kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, nindikie hapo chini katika eneo la comment je wewe umeshaanza kutumia huduma hii au utaanza kutumia hivi karibuni?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.