Mwezi septemba mwaka huu Google itangaza kwamba itafunga huduma yake ya Google Podcast moja kwa moja lakini haikutangaza ni lini itafanya jambo hilo.
Google kwa sasa imeweka wazi kwamba itaachana kabisa kwa kufunga google podcast ikifikia mwezi wa nne kwa mwaka 2024.
Sasa unaweza kujiuliza mbona inaachana na huduma ambayo kwa sasa duniani ina soko kubwa tuu maana kuna huduma nyingi za podcast ambazo zinafanya vizuri tuu.
Kinachoenda kutokea ni kwamba Google wenyewe wameona kuna kauwezo kakuwekeza huduma hiyo ndani ya huduma ya Youtube.
Hii imekaa poa sana kwa maana ya kwamba wanataka kuweka huduma hiyo ya podcast katika huduma ya youtube music.
Na kwa haraka haraka ni kitu kizuri kabisa kama kuna uwezekano wa kupata huduma zote ndani ya mtandao mmoja, hili linafanyika sana hata katika mitandao mingine kama vile Spotify n.k
Google imeanza kupamabana na huduma ya podcast kwa kipindi cha muda mrefu sana na hii ni tokea mwaka 2009 ambapo walianzisha huduma ya Google Listen
Miaka kadhaa imekwenda na wakaja na maboresho kadha wa kadha mpaka kubadilisha jina na kuitwa Google Play Music Podcast na mpaka kufikia katika Google Podcast.
Na kwa sasa mpango ni kusitisha app hiyo na kuihamishia moja kwa moja katika mtandao wa Youtube ambapo mtumiaji atapata vyote kwa wakati mmoja.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je hii umeipokeaje? Unaona ni maamuzi sawa kwa huduma hiyo kuhamia katika mtandao wa Youtube? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.