TikTok ni moja kati ya mitandao ya kijamii yenye majina makubwa sana, licha ya ukubwa wake pia iliweka rekodi kuwa mtandao ambao unakua kwa kasi sana.
Ushawahi kufikiria kama unaweza ukafuta kitu kwa kutumia Google ikiwa ndani ya mtandao wa TikTok? Hili litawezekana kabisa hivi karibuni.
Mara wa mara mitandao mingi imeweka kipengele hichi cha kuweza kutafuta vitu kwa kutumia Google bila hata kutoka nje ya mitandao hiyo.
Kwa sasa jambo hili katika mtandao huo liko katika majaribio na kuhusu kipengele hiki wamechaguliwa watu wachache katika kuhakikisha wanakifanyia majaribio.
#TikTokSearch now displaying external links to Google Search. @MattNavarra pic.twitter.com/cAxNufLA3p
— Radu Oncescu (@oncescuradu) September 19, 2023
Ili kupata kipengele hiki ni lazima uingie katika mtandao wa TikTok na kasha nenda katika sehemu ya kutafuta (search) na kwa chini kabisa utaona kiboksi cha matafuto kutoka Google.
Taarifa zingine zilizopo ni kwamba TikTok pia ina mpango wa kuileta Wikipedia ndani ya mtandao wake huo.
Hii inaonyesha kabisa ni kiasi gani mtandao huo wa kijamii unajitahidi katika kuhakikisha watumiaji wake wanapata kila kitu ndani ya mtandao huo.
Kipengele hiki hakijawekwa wazi kwamba lini kitaanza kupatikana kwa watumiaji wote duniani maana kwa sasa kipo katika hatua za majaribio tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je unadhani ni sawa kwa mtandao wa TikTok kuongeza kipengele cha Google katika mtandao wake?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.