Kampuni la Google kupitia kitengo chake cha ukalimani maarufu kama ‘Google Translate’ sasa kina uwezo wa kutafsiri lugha 103 hiyo ni baada ya kuongeza lugha 13 katika kitengo hicho
Baadhi ya lugha zilizoongezwa ni kihawaii, Kishona, Xhosa, lugha zingine kutoka uarabuni na zingine nyingi. Lakini kwa kuwa lugha hizi zingine zinatumika sehemu ndogo sana duniani ukilinganisha na kiingereza au hata kichina, uongezwaji wake unasaidia kukuza huduma ya Google Translate kwa sababu licha ya udogo wake lazima baadhi ya watu wataitumia na huo ndio uzuri wa teknolojia (kurahishisha maisha).
Wazo la kuanzisha Google Translate lilikuja mwaka 2004 baada ya mmoja kati ya waanzilishi wa Google (Sergey Brin) baada ya kutopendezwa na ‘software’ ya ukalimani ambayo kampuni ilikua ikitumia kwa kipindi hicho.
Bw. Brin sikumoja akawa anasoma meseji iliyoandikwa kwa kikorea kitu ambacho hakikumfurahisha ilikua inasoma “The sliced raw fish shoes it wishes. Google green onion thing!” kwa haraka haraka ni kwamba ‘software’ hiyo ilishindwa kuleta tafsiri ya ukweli.
Hapo awali Google Translate ilikua imejikita katika kutafrsiri lugha chache yaani Kiingereza, Kichina, Kiarabu na Kirusi tuu. Lakini kama kawaida ya Google huwa hawalali, hivyo leo lugha zipo 103 na cha aina yake hapa ni kwamba zamani kampuni hilo lilikuwa likitumia mashine tuu katika kugundua tafsiri mbalimbali, lakini kwa sasa linatumia watu pamoja na mashine hizo.
Lakini pia Google kama kampuni haikufikia mafanikio yake ya sasa kwenye Google Translate yenyewe kama yenyewe. Pia ilipata msaada wa watumiaji wa huduma hiyo ambao wanahusika na ukalimani. Watumiaji hawa walisaidia katika kukua kwa huduma na pia kuongeza lugha nyingine katika huduma. Taarifa zinasema kuwa zaidi ya watu milioni 3 wameongeza tafsiri milioni 200 katika huduma hiyo,