Inajulikana kwamba huduma ya Google Translate inatumika kama ni sehemu moja wapo ya kutafrisi lugha moja kwenda katika lugha nyingine.
Huduma hii –Google Translate– imekua ni msaada mkubwa sana hasa kwa wale ambao wanatumia App hii katika sehemu ambazo wanatumia lugha tofauti au hata ukitakua kujua neno fulani kwa lugha nyingine.
Huduma hii inamilikiwa na kampuni ya Google na mara kwa mara kampuni imekua ikifanya maboresho kama vile kuongeza lugha katika huduma hiyo.
Kwa sasa Google Translate inakuja na lugha 33 ambazo utaweza kuzitumia hata kama uko offline yaani utakua na uwezo wa kutumia lugha hizo hata kama hauna mtandao/intaneti.
Lugha ambazo zimeongezwa ni kama zifuatazo
- Basque
- Cebuano
- Chichewa
- Corsican
- Frisian
- Hausa
- Hawaiian
- Hmong
- Igbo
- Javanese
- Khmer
- Kinyarwanda
- Kurdish
- Lao
- Latin
- Luxembourgish
- Malagasy
- Maori
- Myanmar (Burmese)
- Oriya / Odia
- Samoan
- Scots Gaelic
- Sesotho
- Shona
- Sindhi
- Sundanese
- Tatar
- Turkmen
- Uyghur
- Xhosa
- Yiddish
- Yoruba
- Zulu
*lugha hizi hazipo katika Kiswahili
Google wenyewe wametoa taarifa hii kupitia katika mtandao wao wenyewe kwa njia ya majukwaa ya Google Translate
Kinachofanyika hapa ni kwamba mtumiaji atakua na uwezo wa kushusha (kudownload) baadhi ya lugha wakati akiwa na mtandao au hata WiFi na kisha anaweza akawa anatumia lugha hizo hata akiwa hana huduma ya intaneti.
Cha muhimu kujua hapa ni kwamba kuna baadhi ya lugha ambazo zimetengwa zinawezekana katika kipengele hiki huku zingine haziwezekani.
Soma kila kitu kuhusu Google Translate >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je ushawahi kutumia huduma hii ya Google Translate?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.