Mtandao maarufu wa Google umeleta kwa mara ya kwanza milio ya wanyama katika app za simu na pia kompyuta, kwa kuanzia wamewekwa wanyama 19 ambao mtumiaji anaweza kusikilliza sauti zao kutoka ukurasa wa Search.
Huduma hii ni mpya iliwekwa mwezi wa kwanza katikati lakini haikuwa imepata kuvuma baina ya watumiaji mpaka mwishoni mwa wiki inayoisha.
Ni ukweli usiofichika kwamba kwa namna moja ama nyingine Google imekuwa ikitawala maisha yetu ya kila siku, wanafunzi, walimu, wanamuziki na kila mtu kwa nafasi moja ama nyingine anautegemea mtandao huu. Google wamekuwa wakijitahidi kufanya ubunifu mara kwa mara ili kujihakikishia kuendelea kuwa namba moja.
![milio ya wanyama](https://teknokona.com/wp-content/uploads/2016/03/animal-sounds-desktop-1-1024x799.jpg)
Kwa sasa wanafunzi na watu wengine wanaojifunza juu ya wanyama fulani hawata kuwa na wakati mgumu pindi wanapotaka kujua je mnyama huyo analiaje, watakachotakiwa ni kuiuliza sauti za wanyama Google iwe ni kwenye simu ama kwenye mtandao.
Huduma hii ipo katika lugha ya Kiingeleza na nyingine chache, hivyo ukitaka kuitumia kwa sasa basi ni lazima ujue kimombo, ukiandika tu animal sounds sehemu ya ku-search Google basi itakuletea wanyama tofauti nawe unaweza kumtafuta mnyama unayetaka kuujua mlio wake.
![milio ya wanyama](https://teknokona.com/wp-content/uploads/2016/03/animal-sounds-573x1024.jpg)
Kabla ya google kuleta hii huduma ilimlazimu mtumiaji aende kutafuta mtandaoni clip yenye mnyama husiku ili kusikia mlio wake ama kwa kwenda katika mitandao maalumu ambayo inatoa huduma ya milio ya wanyama. Ujio wa huduma hii Google unarahisisha upatikanaji wa huduma hii kwa watumiaji zidi ya bilioni moja wa mtando wa Google.
Kwa kuanzia kuna sauti ama milio ya wanyama kumi na tisa tuu, tunategemea kwamba Google wataongeza idadi ya wanyama siku zijazo. Pamoja na wanafunzi huduma hii itakuwa ya manufaa kwa wanasanyansi na watafiti hasa wa wanyama.