Tulishaandika kuhufu mradi wa Google ufahamikao kwa jina la Android One. Kwa kifupi kabisa ni harakati za Google kuwezesha upatikanaji wa simu janja zenye toleo la kisasa kabisa la Android, zenye viwango vizuri na kuuzwa kwa chini ya dola 100 za kimarekani (yaani takribani Tsh 200,000/=).
Google kwa ushirikiano na kampuni ya utengenezaji simu ya Infinix wametengeneza simu janja ya kuvutia itakayouzika kwa takribani dola 87 nchini Naijeria, na kupatikana katika nchi nyingine tano kupitia mtandao wa kimauzo wa Jumia. Nchu hizo tano ni Egypt, Morocco, Ghana, Ivory Coast, pamoja na Kenya. Mtandao wa Jumia unapatikana pia Tanzania na hivyo haitakuwa ajabu kama muda si mrefu simu hiyo ikaweza kupatikana na Tanzania pia.
Simu hiyo inayotambulika kwa jina la Infinix HOT 2 inakuja na sifa zifuatazo;
- Inakuja na toleo la Andorid 5.1.1 Lollipop ila siku zijazo utaweza kusasisha (update) kwenda toleo jipya la Android 6.0 Marshmallow
- Toleo hili linakuja katika rangi 5, nyeusi, nyeupe, bluu, nyekundu na ya dhahabu.
- Matoleo ya rangi nyingize zote yanakuja na RAM ya GB1 lakini za rangi ya dhahabu zitakuwa na GB 2
- Kioo cha inchi 5, kiwango kizuri tu cha HD kwa pixels 720 x 1280
- Prosesa ya kiwango cha kati kwa matumizi ya kawaida ya simu, ‘quad-core 1.3 GHz MediaTek processor’
- Uwezo wa laini mbili
- Kamera ya nyuma inakuja na MP 8 wakati ya kupiga selfi inakuja na MegaPixels 2.
- Diski uhifadhi ya ndani (internal memory) ina kiwango cha GB 16
Lengo la simu hizi si kushindana sana na simu za bei ghari kutoka Samsung na watengenezaji wengine wa simu za bei ghari, lengo kuu ni kuhakikisha wengi ambao hawana pesa za kuweza kumiliki simu janja yenye kiwango kizuri na inayotumia toleo jipya kabisa la Android. Wengine pia wanaona ni kama juhudi za Google kuweza kupata watu wengi zaidi mitandaoni ili waweze kupata wateja wengi zaidi katika biashara ya matangazo ya mitandaoni.
Baada ya kuiona simu hii je ungefikiria kuinunua kama ingekuwa inapatikana Tanzania? Tuambie kwa nini?
[socialpoll id=”2289406″]
No Comment! Be the first one.