Ni wazi kwamba kwa sasa simu inayosubiriwa kwa hamu kutoka Google ni Google Pixel 8 na Google kama kawaida yao wamewashangaza wengi.
Kumbuka Google Pixel 8 bado haijawekwa wazi kwa kutambulishwa rasmi na kampuni lakini cha kushangaza ni kwamba Google imeivujisha simu hiyo.
Hii inaweza ikawa inashangaza sana lakini ni kawaida kabisa kwa kampuni ya Google kuvujisha mara kwa mara bidhaa zake ambazo zinakua bado hazijatangazwa.
Kwa mfano kwa Pixel Pro ni bado haijawekwa wazi jinsi ilivyo na pia bado hata sifa zake za undani hazijulikani kabisa maana kwa sasa zinapatikana fununu tuu.
Simu hii imevuja kwa mfumo wa tangazo ambapo likionesha mwanaume mmoja akiwa anaongea na simu (Pixel 8 Pro).
Wengi wanasema simu hiyo ni Pixel 8 pro kwa sababu simu hiyo imeendana kabisa na picha ambazo zilitoka kipindi cha picha za fununu.
Picha hiyo ya simu haina utofauti mkubwa sana na matoleo mengine ya Pixel — hili ni wazi kabisa maana matoleo mengi ya pixel yanafanana.
Ukiachana na uwezo wake mkubwa wa ufanisi, Google Pixel ni moja kati ya simu janja ambazo zinakubalika sana kwa uwezo wake wa kamera.
Kingine ni kwamba uvujishaji huo hauongelei lolote kuhusiana na simu hiyo (bali unaonyesha picha tuu) kwa nyuma.
Hapa ili kupata taarifa kamili ambazo zinaelezea kila kitu hatuna budi kusubiri mpaka Google wenyewe wafanye uzinduzi wa simu hii.
Ningependa kusikia kutoka kwakom niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani ni vizuri kwa Google kuendelea kutumia njia hii ya kuvujisha vitu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.