Yakiwa masaa machache kabla ya filamu ya Starwars haijazinduliwa Google wameamua kuwaburudisha mashabiki wa filamu hiyo kwa kutengeneza gemu spesheli ambayo unaweza kucheza kwa kutumia simu yako (kama panga ) kuzuia miale ya moto unayopigwa na adui katika kompyuta yako.
Filamu ya star wars inamuonesha Han Solo na jeshi lake wakipigana na maadui, moja ya silaha zinazotumika humu ndani inaitwa Lightsaber. Lightsaber ndiyo imekua kama alama ya filamu hii kwa mashabiki wake.

Google wamehamasishwa na ushabiki wa wapenda filamu hiyo juu ya Lightsaber na kuamua kushirikiana na watengenezaji wa filamu hii ili kutengeneza gemu kwa ajiri ya mashabiki wa filamu hii hasa siku hizi chache kabla ya filamu hii kuanza kuoneshwa katika majumba ya sinema.
Mahitaji ya kucheza gemu hili.
- Unahitaji kuwa na Kompyuta iliyounganishwa kwenye mtandao.
- Unahitaji simu nayo yenye mtandao ambayo utaitumia kama siraha (Lightsaber).
Jinsi ya kucheza gemu hili.
Ukitaka kucheza gemu hili basi utahitaji kwenda katika browser yako nakufungua https://lightsaber.withgoogle.com/experience
Kwenye kompyuta yako ndiko mambo yote yanakofanyika isipo kuwa tu kwamba siraha yako inayoonekana katika kompyuta yako hauitumii kwa kuchezesha mouse yako bali kwa kuchezesha simu yako. Unatakiwa uishike simu yako kwa mikono miwili kama vile unavyoshika upanga kupigana na adui, kila ambapo maadui watakupiga na siraha zao wewe unatakiwa kuchezesha simu yako na badala yake upanga unaoonekana katika kompyuta utacheza kama ulivyochezesha simu yako.

Teknokona tunaamini kwamba hii teknolojia ya kutumia simu yako kuchezea siraha badala ya mouse itaweza kuendelezwa na kutumiwa kwenye magemu mengine hapo baadae na pengine kubadilisha kabisa mfumo wa magemu na uchezwaji wake.
Magemu kama Need for Speed ama FIFA pengine nayo yatabadilika jinsi ambavyo yanachezwa iwapo hii teknolojia itaweza kukuzwa na kutumika katika magemu mengine, ni bado mapema kusema ni kwa kiasi gani teknolojia hii itaweza kubadilisha utaratibu uliopo sasa.
Tunatumaini utajaribu gemu hili na utatuambia umejisikiaje kutumia simu yako kama kichezeshea gemu badala ya mouse/kipanya!
No Comment! Be the first one.