Google imetoa kiasi cha dola milioni 100 ili kuinunua kampuni changa inayoitwa Alter ambayo inajihusisha sana sana na teknolojia ya artificial intelligence (AI).
Ni wazi kwa sasa ni makampuni mengi yanajihusisha na teknolojia hii hata kwa haya makampuni mengine makubwa kama Facebook n.k mengi yamejikita katika teknolojia hii.

Sababu kuu ikiwa dunia ndio inahamia katika mfumo huo wa teknolojia, kampuni ya Alter pengine inaweza ikawa ni ngeni katika masikio yako.
Alter inajihusisha sana sana katika kutengeneza Avator (katuni zinazofanania na mtu) ambazo huwa tunazitumia katika mitandao yetu ya kijamii na hata ndani ya magemu.
Kingine ni kwamba jambo hili limefanikishwa miezi miwili iliyopita lakini halikuwekwa wazi katika hadhara na mpaka sasa hakuna taarifa ya kina kabisa kuhusiana na vitu vya ndani ya mauziano haya.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyazfa za juu kabisa katika mtandao wa Alter walionyesha kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kuwa wamepata kazi mpya katika kampuni ya Google kabla ya hata google hawajaweka wazi kuwa wameinunua kampuni hiyo.
Kabla kampuni haijabadilisha jina na kujiita Alter mara ya kwanza kabisa ilikua ikijiita Facemoji, mpaka hapo unaweza ukawa unajiuliza ni kwa nini Google imeinunua kampuni hii.

Ukiachana na hilo tuu, Google ina bahati mbaya na mitandao ya kijamii, huwa ikianzishwa haifanyi vizuri kama mitandao mingine ya kijamii, nadhani unaikumbuka Google+ (Google Plus).
Lakini kingine ni kwamba Google ni kampuni kubwa na nahisi hivi karibuni tuu itafahamika ni wapi teknolojia hii itaenda kutumika ndani ya himaya ya Google.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani ni manunuzi sahahi kwa kampuni kwa sasa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.